TheTanzaniaTime

Kesi Ya Mgawanyo Wa Mali Chadema, Mbivu Mbichi Ya Lissu Leo

2026-02-17 - 08:19

Kesi ya mgawanyo wa mali iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohammed na wenzake wawili inatarajiwa kuendelea asubuhi hii Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam mbele ya Jaji Hamidu Mwanga. Leo yanatarajiwa kusikilizwa mapingamizi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na upande wa walalamikaji wakikataa kuunganishwa kwa Lissu kwenye kesi hiyo kama mdaiwa Ikumbukwe wadaiwa katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika na Bodi ya Wakurugenzi CHADEMA, hivyo kama mapingamizi ya walalamikaji yakikubaliwa Lissu hatojumuishwa katika kesi hii na endapo yatatupiliwa mbali Lissu atakuwa mshtakiwa. Pamoja na mambo mengine Lissu katika kesi hii hana Wakili hivyo anajitetea mwenyewe.

Share this post: