Kamati Ya Bunge Yapokea Wasilisho La Miradi Ya Wizara Ya Habari
2026-03-10 - 22:18
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepokea taarifa ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Taasisi zake. Taarifa hiyo iliwasilishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma Machi 10, 2026 Bungeni Jijini Dodoma. Baada ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Husna Sekiboko alisema hatua inayofuata ni kufanya ziara ya kuona utekelezaji katika miradi hiyo.
Share this post: