TheTanzaniaTime

Kamati ya Bunge; OSHA Italipunguzia Taifa Mzigo wa Fidia na Matibabu

2026-02-14 - 18:21

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imesema majukumu ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) yakitekelezwa ipasavyo yatalipunguzia Taifa mzigo wa kuhudumia wananchi wanaoweza kuumia au kupata magonjwa yatokayo na kazi. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hawa Chakoma, alipokuwa akihitimisha mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa na OSHA kwa wajumbe wa Kamati hiyo Februari 12, 2026. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa na OSHA kwa Kamati hiyo Bungeni Jijini Dodoma. Mafunzo hayo ya siku moja ambayo yamefanyika bungeni Jijini Dodoma ni utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Kamati hiyo katika kikao cha Januari 19, 2026 OSHA ilipowasilisha taarifa kuhusu muundo na majukumu yake. Mafunzo hayo yanalenga kuiwezesha Kamati hiyo kutekeleza ipasavyo jukumu lake la kuisimamia Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) na Taasisi chini yake ikiwemo OSHA. Mheshimiwa Chakoma ameipongeza Taasisi ya OSHA kwa jitihada inazofanya kutekeleza majukumu yake ikiwemo kutoa mafunzo kwa waaajiri na wafanyakazi, kufanya ukaguzi wa mifumo ya usalama na afya ukiwemo uchunguzi wa afya za wafanyakazi katika hatua mbalimbali. Mkaguzi wa Mazingira ya Kazi na Afisa Mafunzo kutoka OSHA, Simon Lwaho, akiwasilisha mada kuhusu vihatarishi vya usalama na afya katika mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Bungeni Jijini Dodoma. “Niendelee kuwapongeza pamoja na kuwashukuru kwa mafunzo haya ambayo yamewafungua wabunge wengi na kimsingi ni mafunzo mazuri ambayo ukiyaangalia kwa haraka haraka unaweza kudhani ni kwa ajili ya maeneo ya kazi tu lakini kiukweli unaweza kuyatumia hata katika mazingira ya nyumbani kwenye hatari tofauti tofauti,” ameeleza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii na kuongeza: “Mafunzo haya ni kwa ajili ya kuimarisha afya za wafanyakazi na wananchi kwa ujumla na sote tunakuballiana kwamba OSHA ipo kwa ajili ya kuliokoa Taifa ambapo ikifanya kazi yake sawa sawa kwa mujibu wa utaratibu waliotueleza hapa ama hakika tutakuwa tunaliokolea Taifa letu mzingo mzito wa kuwatibia wagonjwa ama kuwapa fidia wafanyakazi waliomia kazini.” Mkufunzi wa Huduma ya Kwanza Mahali pa Kazi kutoka OSHA, Moteswa Meda, akiwasilisha mada katika mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Bungeni Jijini Dodoma. Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda, akitoa ufafanuzi wa masuala na hoja mbalimbali zilizoibuliwa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii baada ya mafunzo ya usalama na afya mahala pakazi,yaliyotolewa kwa Kamati hiyo Bungeni Jijini Dodoma. Sambamba na kuipongeza OSHA kwa kutoa mafunzo mazuri, Kamati hiyo imeitaka OSHA kuwashauri wamiliki wa sehemu za kazi kutumia teknolojia na mitambo ya kisasa iliyosanifiwa katika namna inayopunguza athari nyingi za kiusalama na kiafya wakitolea mfano wa vipando (lift) zilizopo katika majengo marefu katika miji mbalimbali hapa nchini.Aidha, Kamati hiyo imependekeza elimu ya masauala ya usalama na afya kutolewa kwa wabunge wote pamoja na wanachi mbalimbali wakiwemo wakulima wadogo wadogo hususan wanaojishughulisha na kilimo cha tumbaku mkoani Tabora. Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda, akitoa ufafanuzi wa masuala na hoja mbalimbali zilizoibuliwa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii baada ya mafunzo ya usalama na afya mahala pakazi,yaliyotolewa kwa Kamati hiyo Bungeni Jijini Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu akitoa maelezo ya awali kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu mafunzo ya usalama na afya mahala pakazi yaliyoandaliwa na OSHA Kamati hiyo. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu akitoa maelezo ya awali kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu mafunzo ya usalama na afya mahala pakazi yaliyoandaliwa na OSHA Kamati hiyo. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Hawa Chakoma, akihitimisha mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa na OSHA kwa wajumbe wa Kamati hiyo Februari 12, 2026. “Tangu nilipoingia kwenye hii Kamati na kujua kazi zinazofanywa na OSHA natamani kuwaona kila mahali na kupitia mafunzo yetu ya leo OSHA wametoa elimu kubwa sana japo hatukuwa na muda wa kutosha,” amesema Katani Ahmad Katani, Mjumbe wa Kamati. “Niwapongeze OSHA kwa mafunzo mazuri na niungane na wenzangu kusema kuwa mafunzo haya ni muhimu sana na yanaweza kutusaidia sana katika maisha yetu ya kila siku na niombe tuendelee kupatiwa mafunzo kama haya,” ameeleza Mariam Kisangi ambaye ni Mjumbe wa Kamati. OSHA ni miongoni mwa Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano yenye jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003. Miongoni mwa majukumu ya msingi ya OSHA ni kutoa mafunzo ya usalama na afya kwa waajiri, wafanyakazi na umma kwa ujumla.

Share this post: