Jinsi ya Kujua Kama Betri ya Simu Yako Ni Original Unaponunua Simu Mpya
2026-02-20 - 03:28
Unaponunua simu mpya, moja ya sehemu muhimu zaidi ni betri. Betri halisi ni uhakika wa maisha marefu ya simu, utendaji thabiti, na usalama wa kifaa chako. Hapa kuna mwongozo wa namna ya kuthibitisha kama battery ni original kabla ya kununua. 1. Nunua Simu Kwa Duka Rasmi au Wakala Aliyeidhinishwa Simu zinazouzwa kwa maduka yasiyo rasmi mara nyingi zinaweza kuwa na betri bandia. Ili kuepuka hatari: Angalia wakala rasmi wa brand (authorized dealer). Epuka ofa za bei “ndogo sana” – mara nyingi ni ishara ya bidhaa zisizo halali. 2. Kagua Ufungashaji wa Simu Battery halisi kawaida huja na simu ambayo imefungwa vizuri: Seal ya boksi iwe thabiti, isiyokuwa imevunjika. Logo na maandishi yawe safi, yasiyo na makosa ya tahajia. Angalia IMEI iliyoko kwenye boksi na kuhakikisha inalingana na ile ya simu (Dial *#06#). 3. Angalia Hali ya Betri Kwenye Settings Kwa simu nyingi za kisasa, unaweza kuangalia afya ya battery bila kufungua kifaa: iPhone: Settings > Battery > Battery Health & Charging Samsung: Samsung Members App > Device Diagnostics Xiaomi: Settings > About Phone > Battery Status Dalili za battery isiyo original: ujumbe wa “Unknown Part” au “Battery Not Genuine”. 4. Kagua Utendaji wa Battery Dalili za battery bandia ni: Kuisha chaji haraka hata bila kutumia simu sana Kuchemka kupita kiasi Asilimia ya battery kuruka kwa ghafla (mfano kutoka 40% hadi 20%) 5. Thibitisha Kupitia Kampuni Husika Brand nyingi hutoa njia za kuthibitisha kifaa: Samsung – Samsung Members App Apple – Settings > Battery Health Xiaomi – MIUI Security Verification Hii inathibitisha kama betri na sehemu nyingine za simu ni halisi.