TheTanzaniaTime

Iran Yatishia Kuzamisha Meli Za Kivita Za Marekani

2026-02-18 - 11:57

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amesema Rais wa Marekani Donald Trump hatofanikiwa kuangamiza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, huku akitoa onyo kali dhidi ya Marekani na kutishia kulenga manowari ya kijeshi ya Marekani iliyoko katika eneo la Mashariki ya Kati endapo mvutano utaongezeka. Khamenei alisisitiza kuwa Iran iko tayari kujilinda dhidi ya shinikizo lolote la kijeshi au kisiasa kutoka Washington, akisema taifa lake haliwezi kutishwa wala kulazimishwa kukubali masharti ya Marekani. Kauli hiyo kali ya Khamenei imetolewa wakati mazungumzo ya raundi ya pili kati ya Marekani na Iran kuhusu mpango wa nyuklia yakihitimishwa mjini Geneva, Switzerland. Ripoti kutoka vyombo vya habari zinasema misafara iliyokuwa imewabeba wajumbe wa pande zote mbili imeondoka katika eneo la mazungumzo, ishara kwamba majadiliano hayo yamefikia tamati baada ya siku kadhaa za mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja.

Share this post: