TheTanzaniaTime

Iran Yalenga Maeneo 8 Israel Katika Mashambulizi ya Makombora – Video

2026-03-23 - 08:34

Iran imezidisha mashambulizi yake ya makombora dhidi ya Israel kwa kutumia makombora ya cluster, yakilenga maeneo nane tofauti katika sehemu za kati na kusini mwa nchi hiyo katika operesheni ya usiku iliyosababisha taharuki kubwa. Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika ni Mji wa Rishon LeZion, ambako taarifa zinaeleza kuwa kombora moja lilianguka karibu na shule ya chekechea, tukio lililozua hofu kubwa kutokana na uwezekano wa madhara kwa watoto na familia zilizo karibu. Mashambulizi hayo yalienea pia katika miji mikubwa ya Tel Aviv na Jerusalem, ambako ving’ora vya tahadhari vililia kwa muda mrefu usiku mzima. Wakazi walilazimika kukimbilia kwenye mahandaki na vyumba vya usalama huku baadhi wakikesha humo kutokana na hofu ya mashambulizi ya mfululizo. Kwa mujibu wa Jeshi la Israel (IDF), mfumo wa ulinzi wa anga uliweza kudungua takribani asilimia 90 ya makombora yote yaliyorushwa. Hata hivyo, matumizi ya makombora ya cluster yamefanya hali kuwa hatari zaidi, kwani hata makombora yanapodunguliwa angani, hubaki yakitawanya vipande na vilipuzi vidogo (submunitions) vinavyoanguka katika maeneo makubwa ya makazi. Katika maeneo kadhaa, vipande vya makombora (shrapnel) vilivyoanguka vimesababisha moto katika majengo ya makazi, magari, na miundombinu ya umeme. Vikosi vya zimamoto viliripotiwa kupambana na moto katika maeneo tofauti kwa wakati mmoja, hali iliyoonyesha ukubwa wa athari za mashambulizi hayo. Aidha, baadhi ya makombora ya cluster ambayo hayakudunguliwa yalilipuka ardhini na kutawanya vilipuzi vidogo vilivyoharibu nyumba na kusababisha majeruhi kwa raia. Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

Share this post: