Historia Yajirudia! Tyla Ashinda Grammy Tena 2026
2026-02-02 - 14:39
Msanii wa kimataifa kutoka Afrika Kusini, Tyla, ameendelea kuandika historia mpya katika muziki wa Afrika baada ya kushinda tuzo yake ya pili ya Grammy kwenye kipengele cha Best African Music Performance katika Tuzo za Grammy 2026. Ushindi huu umechukuliwa kama hatua kubwa kwa muziki wa Afrika, huku ukithibitisha ukuaji na ushawishi wa wasanii wa bara hilo katika jukwaa la kimataifa. Mafanikio ya Tyla yanazidi kuwa ya kipekee hasa ikizingatiwa kuwa aliwashinda wapinzani wake wakubwa kutoka Nigeria, taifa ambalo kwa muda mrefu limekuwa likitawala majukwaa mengi ya muziki wa Afrika duniani. Katika kipengele hicho, Tyla alikuwa akishindana na majina mazito yakiwemo Burna Boy, Davido akishirikiana na Omah Lay, Ayra Starr akimshirikisha Wizkid, pamoja na Eddy Kenzo kutoka Ugandawasanii wenye rekodi na ushawishi mkubwa barani Afrika na nje ya bara hilo. Hii inakuwa mara ya pili kwa Tyla kushinda tuzo hiyo, baada ya ushindi wake wa kwanza mwaka 2024, ambapo aliweka historia kwa kuwa msanii wa kwanza kabisa kushinda kipengele cha Best African Music Performance tangu kilipoanzishwa. Kwa ushindi huu wa pili, Tyla si tu ameweka rekodi, bali pia ameandika ukurasa muhimu katika historia ya muziki wa Afrika kwenye tuzo za Grammy. Orodha Kamili ya Washindi wa Grammy Awards 2026