TheTanzaniaTime

Harmonize Athibitisha Penzi Zito kwa Kajala, Asema ‘Huyu Ndiye Maisha Yangu’

2026-02-05 - 08:48

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa Konde Music Worldwide, Harmonize, ameibua hisia na gumzo kubwa mitandaoni baada ya kuandika ujumbe mzito wa kimapenzi kwa mchumba wake Kajala Frida, wakati wakisherehekea hatua mpya ya uchumba wao. Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Harmonize alimiminika maneno ya shukrani na mapenzi, akimtaja Kajala kama baraka na zawadi maalum kutoka kwa Mungu katika maisha yake. Ujumbe huo umeonyesha upande wake wa hisia na ukomavu, jambo lililogusa mashabiki wengi. Katika sehemu ya ujumbe wake, staa huyo aliandika: “Wewe ni zawadi ya Mungu kwenye maisha yangu... nitakuchagua leo, kesho na milele.” Lakini hakuishia hapo. Harmonize aliendelea kufunguka zaidi kuhusu namna penzi hilo limembadilisha na kumjenga kama mwanaume, akieleza kuwa upendo na heshima anayompa Kajala ndivyo vinavyompa motisha ya kufanya kazi kwa bidii zaidi, kutafuta mafanikio makubwa na kuwa bora kila siku. “Upendo na heshima ninayokupa vinanirudia... nikikupenda najipenda zaidi, nawaza maendeleo zaidi, niwe tajiri zaidi nikutunze vizuri zaidi. Najikuta natoboa mdogo mdogo na nasogea... Alhamdulilah.” Aidha, alieleza kuwa Kajala amemsaidia kubadilika kitabia na kuwa mtu mwenye heshima zaidi katika jamii. “Umenijenga na unaendelea kunijenga niwe gentleman zaidi, naheshimika zaidi because of you wife... kukupenda na kukuheshimu sio promise tena, ni maisha.” Mashabiki wamiminika kwa pongezi Baada ya ujumbe huo kusambaa, mashabiki na watu maarufu walijaa kwenye sehemu ya maoni wakimpongeza kwa uwazi wake wa hisia na kuthamini mwenza wake hadharani. Wengi walitaja penzi lao kuwa mfano wa uvumilivu, kujifunza na kukua pamoja licha ya changamoto walizowahi kupitia. Harmonize alihitimisha kwa maneno ya shukrani na ahadi ya kudumu: “Thanks a lot for trusting and always being at my side... this is my last card kwenye mchezo wa maisha.” Kauli hiyo imewafanya wengi kuamini kuwa safari yao sasa imefika hatua ya uhakika zaidi kuelekea maisha ya ndoa.

Share this post: