TheTanzaniaTime

Halmashauri ya Wilaya ya Songea Yatangaza Nafasi 5 za Ajira

2026-01-26 - 04:21

Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma imetangaza nafasi tano (5) za ajira kwa Watanzania wenye sifa, baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kwa mujibu wa tangazo hilo lililotolewa Januari 22, 2026, ajira hizo ni za Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II, ambapo nafasi zote tano zinahitajika kujazwa mara moja. Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo wa Ajira Portal kwa anuani ya https://portal.ajira.go.tz, ambapo mwisho wa kutuma maombi ni Januari 29, 2026. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu uliobainishwa hayatafanyiwa kazi. Tangazo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, ambaye amewataka waombaji kuzingatia masharti yote ili kuepuka usumbufu. a na elimu ya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita, pamoja na kuhitimu Stashahada au NTA Level 6 katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Aidha, mwombaji anatakiwa kuwa na ujuzi wa matumizi ya kompyuta.

Share this post: