TheTanzaniaTime

Halmashauri ya Mwanga Yatangaza Nafasi 9 za Ajira kwa Watanzania

2026-02-09 - 03:30

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga ametangaza waziwazi fursa za ajira tisa (9) kwa Watanzania wenye sifa, baada ya kupata kibali cha Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Nafasi hizo ni pamoja na: Dereva Daraja la II – Nafasi 5 Mwandishi Mwenda Ofisi II – Nafasi 4 Sifa Muhimu za Waombaji Kuwa raia wa Tanzania na umri si zaidi ya miaka 45. Kwa Madereva: Form IV + leseni ya Daraja E au C na uzoefu wa angalau mwaka 1 bila ajali. Kwa Waandishi Mwenda Ofisi: Form IV au VI + Diploma/Uhazili au NTA Level 6 + ujuzi wa kompyuta na lugha. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba. Masharti ya Jumla Waombaji wote watalazimika kuambatisha C.V, vyeti vya elimu vilivyothibitishwa, na vyeti vya mafunzo husika. Vyeti vya masomo ya nje ya Tanzania lazima viidhinishwe na mamlaka husika (TCU, NECTA, NACTE). Waombaji waliostaafuwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. Mwisho wa kuwasilisha maombi: 20 Februari 2026. Jinsi ya Kuomba Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielectroniki wa Ajira kwa https://portal.ajira.go.tz. Maombi yasiyo tumwa kwa njia hii hayatazingatiwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na: Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, S.L.P 716, Mwanga Simu: +255 26 2757652 | Nukushi: +255 26 2756463

Share this post: