Halmashauri ya Jiji la Mbeya Yatangaza Nafasi 19 za Ajira
2026-03-05 - 03:57
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi kumi na tisa (19) baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kumb. Na: MCC/E.40/5/VOL. II/85 Tarehe: 04/03/2026 1.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 13 Ngazi ya Mshahara: TGS B Majukumu Kukagua gari kabla na baada ya safari Kusafirisha watumishi kwenye safari za kikazi Kufanya matengenezo madogo madogo Kusambaza nyaraka mbalimbali Kujaza na kutunza daftari la safari Kufanya usafi wa gari Kazi nyingine atakazopangiwa na Mwajiri Sifa za Mwombaji Elimu ya Kidato cha Nne Leseni Daraja C au E (angalau mwaka 1 wa uzoefu bila ajali) Cheti cha Basic Driving Course kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali 2.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 6 Ngazi ya Mshahara: TGS C Majukumu Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka Kusambaza na kupokea majalada Kutafuta na kurejesha kumbukumbu Kufuatilia mzunguko wa majalada (file tracking) Kazi nyingine atakazopangiwa Sifa za Mwombaji Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) Stashahada (NTA Level 6) ya Utunzaji wa Kumbukumbu Ujuzi wa Kompyuta Masharti ya Jumla Awe raia wa Tanzania (miaka 18–45) Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba CV yenye anuani, simu, barua pepe na wadhamini watatu Viambatisho vyote viwe vimethibitishwa na Mwanasheria/Wakili “Result slip” na Testimonial hazitakubaliwa Waombaji waliosoma nje ya nchi wathibitishe vyeti (TCU/NACTE/NECTA) Maombi ya kughushi yatachukuliwa hatua za kisheria Maombi yaandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza Mwisho wa kutuma maombi: 17/03/2026 Jinsi ya Kutuma Maombi Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal): https://portal.ajira.go.tz/ Barua ziandikwe na kuelekezwa kwa: Mkurugenzi wa Jiji Halmashauri ya Jiji la Mbeya S.L.P 149 Mbeya Ofisi Kuu: Mtaa wa Maktaba, Mbeya Simu: +255 25 2502372 Nukushi: +255 25 2502488 Barua pepe: cd@mbeyacc.go.tz Tovuti: www.mbeyacc.go.tz