TheTanzaniaTime

Hafla ya Tuzo za Tanzania Creator Kufanyika Leo Mlimani City

2026-02-12 - 15:50

Dar es Salaam – Leo Alhamisi, Februari 12, 2026, macho na masikio ya wadau wa burudani yameelekezwa katika Ukumbi wa Mlimani City Conference Centre, ambako hafla kubwa ya utoaji tuzo za Tanzania Creator inafanyika. Tukio hilo linatarajiwa kukutanisha wasanii maarufu, wadau wa sanaa, wageni waalikwa pamoja na mashabiki wengi, likiwa jukwaa la kutambua na kuenzi mafanikio ya vipaji na mchango wa wadau wa tasnia kwa mwaka uliopita. Miongoni mwa wageni wa heshima watakaohudhuria ni Mbunge wa Buchosa na Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo, jambo linaloongeza uzito na hadhi ya kipekee kwa hafla hiyo. Waandaaji wamesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100, huku burudani za jukwaani, maonesho ya moja kwa moja na utoaji wa tuzo mbalimbali vikitarajiwa kuufanya usiku huo kuwa wa kipekee na wa kukumbukwa. Aidha, mastaa waliothibitisha kuhudhuria ni pamoja na Kajala Masanja, Jokate, Hamisa Mobetto, Kili Paul, Duma, mtangazaji wa Global TV Imelda Mtema, Careen Simba, MC Gara B, Lamata, pamoja na wengine wengi, hali inayotarajiwa kuongeza mvuto mkubwa kwa mashabiki. Kwa wale wasiohudhuria moja kwa moja, hafla hii itakuwa mubashara (live) kupitia Global TV Online, hivyo usikose kushuhudia tukio hili la historia.

Share this post: