TheTanzaniaTime

Global TV Yapiga Hatua Kubwa, Imelda Mtema Ang’ara Kwenye Tuzo za Wildaf – Video

2026-02-06 - 05:50

Mwandishi mkongwe wa habari na mtangazaji wa Global TV, Imelda Mtema. Mwandishi mkongwe wa habari na mtangazaji wa Global TV, Imelda Mtema (@imeldamtema), ameendelea kuthibitisha ubora wake katika tasnia ya habari baada ya kung’ara katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wildaf, zilizolenga kuwatambua vinara wa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia. Imelda alikuwa mmoja wa waongozaji wakuu wa tukio hilo muhimu, akionesha umahiri wake wa uwasilishaji, kujiamini jukwaani pamoja na weledi uliovutia hadhira iliyohudhuria hafla hiyo. Katika hafla hiyo, jumla ya wanaharakati na wadau 16 waliotajwa kuwa mstari wa mbele kupinga na kupambana na ukatili wa kijinsia walitunukiwa tuzo maalum kama ishara ya kuthamini mchango wao kwa jamii. Tuzo hizo zimetolewa Februari 5, 2026, zikilenga kuhamasisha jamii kuendelea kusimama imara kulinda haki za wanawake, watoto na makundi yaliyo katika hatari ya ukatili. Mashabiki na wadau wa tasnia ya habari hawakusita kupongeza uwasilishaji wa Imelda, wakimtaja kama mmoja wa watangazaji wenye mvuto na taaluma ya hali ya juu, hasa katika matukio makubwa yenye hadhi ya kimataifa. Kwa miaka kadhaa sasa, Imelda ameendelea kujijengea jina kama mtangazaji mahiri, mwenye uwezo wa kubeba matukio mazito kwa ufasaha na weledi.

Share this post: