Global TV Yang’ara Mlimani City, Yatwaa Tuzo ya Best Online Tanzania Creator’s Awards – Video
2026-02-13 - 08:10
Global TV imeibuka mshindi katika kipengele cha Best Online Media kwenye Tanzania Creators Awards 2025 zilizofanyika Februari 12, 2026, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kupitia ushindi huo, Global TV imetambuliwa kwa mchango wake katika utoaji wa habari sahihi, za haraka na zenye ubunifu kupitia majukwaa ya kidijitali, ikiendelea kujiimarisha katika tasnia ya habari na burudani nchini. Baada ya kutangazwa mshindi, uongozi wa kituo hicho ulitoa shukrani kwa watazamaji na wafuasi wake kwa kuendelea kukiunga mkono, ukieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na imani na ushirikiano wa karibu kati ya kituo na jamii. @creators_awards ni jukwaa linalolenga kutambua na kuthamini wabunifu pamoja na vyombo vya habari vinavyochangia mabadiliko chanya kupitia maudhui ya kidijitali, huku likihamasisha ukuaji wa tasnia ya mawasiliano nchini.