Ford Yampa Papa Leo XIV Zawadi ya Gari Maalum la 2026 Ford Explorer
2026-03-16 - 09:26
Mkurugenzi Mkuu wa Ford Motor Company, Jim Farley, amemzawadia Papa Leo XIV gari la kipekee aina ya Ford Explorer Platinum Hybrid 2026 lililotengenezwa maalum katika kiwanda cha Chicago nchini Marekani. Zawadi hiyo maalum ilitolewa kama ishara ya heshima kwa Papa huyo ambaye ni wa kwanza kuzaliwa nchini Marekani kuongoza Kanisa Katoliki. Gari hilo limepambwa kwa nakshi maalum zinazoonyesha muunganiko wa mji wa Chicago na Vatican City, zikiwemo michoro ya mandhari ya majengo marefu (skyline) ya miji hiyo miwili. Mbali na hilo, gari hilo lina namba za kipekee za usajili zilizoandikwa “DA POPE”, jambo linalolifanya kuwa zawadi ya kipekee inayochanganya imani, utamaduni na ubunifu wa teknolojia ya kisasa. Gari hilo liliwasilishwa rasmi kwa Papa mnamo Februari 28, 2026, kama alama ya uhusiano kati ya imani ya kidini na ubunifu wa viwanda vya kisasa.