TheTanzaniaTime

Farhan Afunguka Mo Dewj Kuchafuliwa, Ishu ya Mangungu Kupigwa

2026-02-07 - 14:39

Mwandishi wa habari na mchambuzi mahiri wa masuala ya michezo, Farhan Kihamu, amezungumza na Global TV kufuatia sakata la baadhi ya mashabiki wa klabu ya Simba kudaiwa kutaka kumshambulia Mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu. Aidha, Farhan amegusia sakata lingine la mashabiki kuitisha mkutano na waandishi wa habari, wakiiibua tuhuma na hoja nzito dhidi ya mwekezaji wa klabu hiyo, Mo Dewji. Katika mazungumzo hayo, Farhan Kihamu ameeleza kuwa mafanikio makubwa yaliyoipata klabu ya Simba yamechangiwa kwa kiwango kikubwa na uwekezaji wa Mo Dewji. Ameeleza kushangazwa na baadhi ya mashabiki wanaomkosoa mwekezaji huyo, akitolea mfano wa mafanikio yanayooneshwa na mwekezaji wa klabu ya Yanga, Ghalib Said Mohammed (GSM), akisisitiza kuwa hatua na mafanikio hayo yalishawahi kufikiwa na Simba chini ya uwekezaji wa Mo Dewji takribani miaka mitano iliyopita.

Share this post: