Fahamu Madhara Yatokanayo na Kufungwa kwa Strait of Hormuz Duniani
2026-03-03 - 08:18
Strait of Hormuz ni njia nyembamba ya bahari yenye umuhimu mkubwa duniani. Ina upana wa takribani maili 30 katika sehemu yake nyembamba zaidi, ikiwa kati ya Rasi ya Musandam (Oman) na pwani ya Iran. Njia hii inaunganisha Ghuba ya Uajemi na Ghuba ya Oman, na hivyo kuwa mlango muhimu wa usafirishaji wa mafuta na gesi duniani. Kwa kawaida, meli za kibiashara hupita kupitia mfumo maalum unaoitwa Traffic Separation Scheme (TSS) uliopo kaskazini mwa Oman. Mfumo huu hupanga njia za kuingia na kutoka ili kupunguza ajali na msongamano wa meli. Eneo hili lina kina kinachofikia zaidi ya futi 650. Mafuta mengi yanayopita hapa hutoka katika nchi za Ghuba, zikiwemo: Saudi Arabia Iraq Kuwait United Arab Emirates Qatar (hasa gesi asilia – LNG) Iran Nchi hizi husafirisha mafuta yao kwenda Asia, Ulaya, Marekani na maeneo mengine kupitia njia hii. Madhara yatokanayo na kufungwa kwa Strait of Hormuz Kufungwa kwa mlango huu muhimu wa bahari kunasababisha athari kubwa kimataifa, hasa kiuchumi na kiusalama: 1⃣ Kupanda kwa bei ya mafuta duniani Sehemu kubwa ya mafuta ya dunia husafirishwa kupitia hapa. Kufungwa kwake kunasababisha uhaba wa mafuta sokoni. Bei ya mafuta na gesi inapanda haraka, na kuathiri gharama za usafiri, umeme na bidhaa nyingine. 2⃣ Mshtuko wa uchumi wa dunia Nchi zinazotegemea mafuta kutoka Mashariki ya Kati zinakumbwa na changamoto kubwa. Masoko ya hisa yanatikisika. Mfumuko wa bei ungeongezeka katika nchi nyingi. 3⃣ Migogoro ya kijeshi Eneo hili ni nyeti kijeshi. Kufungwa kunaweza kusababisha mvutano au mapambano kati ya mataifa yenye maslahi ya kiuchumi na kiusalama katika eneo hilo. Ulinzi wa meli za kibiashara ungeongezwa. 4⃣ Kuathirika kwa usafirishaji wa kimataifa Si mafuta tu yanayopita hapo, bali pia gesi asilia (LNG) na bidhaa nyingine. 5⃣ Athari kwa nchi za Ghuba Nchi kama Saudi Arabia, UAE, Kuwait, Qatar na Iraq zinapoteza njia yao kuu ya kuuza mafuta. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa za bahari, ni njia ya kimataifa ya usafiri (international waterway), hivyo meli za kibiashara zina haki ya kupita. Strait of Hormuz Haumilikiwi na nchi moja, lakini inapakana moja kwa moja na Iran na Oman.