TheTanzaniaTime

Fahamu Hadithi ya Zein Al-Dalou: Msichana Asiyeona Aliyehifadhi Qur’ani Wakati wa Vita Gaza – Video

2026-03-06 - 16:07

Katika giza lisilo na mwisho... alizaliwa msichana asiye na macho ya kuona dunia.Lakini moyo wake ulikuwa umejaa nuru ya Qur’ani, kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu. Licha ya kupoteza uwezo wa kuona tangu kuzaliwa, msichana asiyeona mwenye umri wa miaka 16 aitwaye Zein Al-Dalou aliweza kukamilisha kuihifadhi na kuisoma Qur’ani Tukufu yote wakati wa vita vinavyoendelea katika Ukanda wa Gaza, akivumilia na kushinda mazingira magumu ya kibinadamu. Zein alizaliwa bila mboni za macho, na baadaye alifanyiwa matibabu ikiwemo kuwekwa macho ya bandia, baada ya mama yake kuvuta moshi wa fosforasi nyeupe wakati wa mashambulizi ya kijeshi ya Israeli dhidi ya Ukanda wa Gaza mwaka 2009. Licha ya hali hiyo, Zein anaendelea na masomo yake kwa azma na uthabiti mkubwa, akitumia kifaa cha maandishi cha Braille chenye vitufe sita, kinachomwezesha kuandika na kusoma katika lugha mbalimbali za duniani. Mafanikio yake yanathibitisha kuwa ulemavu haujawahi kuwa kizuizi kwa ndoto na malengo yake. Hadithi yake inatukumbusha kitu kimoja muhimu: Wakati mwingine macho hayaoni... lakini moyo ndio unaona zaidi. Kwa Zein, ulemavu haukuwa mwisho wa ndoto bali mwanzo wa ushindi!

Share this post: