TheTanzaniaTime

Epstein Files: Ushahidi Mpya Wazua Mshituko Duniani, Waonesha Epstein Aliuawa Gerezani Kuokoa Mabilionea Wengine – Video

2026-02-18 - 10:07

Wiki hii, nyaraka mpya zimeibuka nchini Marekani. Nyaraka ambazo zimezua mjadala mkubwa duniani. Baadhi ya wachunguzi sasa wanaamini kuna ushahidi unaoongezeka unaoonyesha kuwa kifo cha Jeffrey Epstein huenda hakikuwa kujiua... bali mauaji yaliyopangwa. ALIUAWA! Lakini ili kuelewa uzito wa Makala haya, lazima turudi nyuma kidogo. Jeffrey Epstein alikuwa bilionea mkubwa nchini Marekani aliyekuwa na marafiki wengi wenye nguvu duniani. Julai 6 Mwaka 2019 alikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kufanya biashara ya ngono na unyanyasaji wa kingono wa watoto wadodo – stori ni ndefu sana kwenye hili sakata. Akiwa bado mahabusu, Agosti 10, 2019 Epstein alikutwa amekufa katika selo yake ndani ya gereza lenye ulinzi mkali jijini New York, Marekani – ikiwa ni ndani ya mwezi mmoja tu tangu akamatwe kufunguliwa mashitaka hayo. Serikali ilisema: alijiua kwa kutumia shuka. Lakini tangu siku hiyo... dunia haijawahi kuamini kikamilifu stori hiyo. Sasa, baada ya mamilioni ya kurasa za nyaraka mpya kutolewa na United States Department of Justice, maswali yanaongezeka kuliko majibu. Je, ni kweli Epstein alijiua? Au aliuawa ili asiweze kufichua siri za watu wenye nguvu aliokuwa akishirikiana nao? Kwani nyaraka nyingi zinataja majina makubwa kama Donald Trump, Baraka Obama, Elon Musk, vigogo kutoka famle za kiarabu, Uingereza na wengine kibao... SEHEMU YA 1: SIKU EPSTEIN ANAKUTWA AMEUAWA KWENYE SELO YAKE, USHAHIDI MPYA UNAONESHA MTIRIRIKO WA MATUKIO ULIKUWA KAMA IFUATAVYO: Kwenye kamera za ulinzi wa gereza la Manhattan, wachunguzi waliona kitu kisichoeleweka. Ni kama mwanga hafifu wa rangi ya machungwa ukipanda ngazi kuelekea sehemu iliyokuwa na selo ya Epstein. Muda ulikuwa saa 4:39 usiku — wafungwa wote walipaswa kuwa wamefungiwa. Masaa machache baadaye, Epstein anakutwa amaelala chini amenyooka, hajitambui. Kwa mujibu wa nyaraka zilizotolewa na Idara ya Haki ya Marekani, wachunguzi waliokuwa wakikagua video za kamera za ulinzi za usiku ambao Epstein alikutwa amekufa, waliona kitu kisichoeleweka: umbo hafifu la rangi ya machungwa likipanda ngazi kuelekea sehemu ya gereza (inayojulikana kama tier) iliyokuwa na selo ya Epstein. Wafungwa katika gereza hilo walikuwa wanapewa mavazi na mashuka ya rangi ya machungwa. Hata hivyo, tukio hilo lilionekana saa 4:39 usiku, wakati ambao wafungwa wote walipaswa kuwa tayari wamefungiwa ndani ya vyumba vyao. “Mwanga huo wa ajabu wa rangi ya machungwa” ni miongoni mwa maelezo mengi yaliyofichuliwa katika nyaraka mpya za kesi ya Epstein, ambayo yanaendelea kuongeza mashaka kuhusu simulizi rasmi kwamba alijiua. Swali linabaki: Nani alipanda ngazi usiku huo? SEHEMU YA 2: Makubaliano ya Siri Kabla ya Kifo Wiki chache kabla ya kifo chake, mawakili wa Epstein walikuwa wakijadili uwezekano wa ushirikiano na serikali. Kwa lugha rahisi: Inawezekana alikuwa tayari kuwataja watu wengine ili apunguziwe adhabu. Epstein alikuwa na marafiki wengi wenye nguvu — wanasiasa, wafanyabiashara na watu mashuhuri duniani. Je, kuna waliogopa angezungumza? SEHEMU YA 3: Jaribio la Kwanza la “Kujiua” Julai 23, 2019 — Epstein alipatikana na kitambaa shingoni. Alisema alishambuliwa. Mfungwa mwenzake alisema alimsaidia. Siku iliyofuata alimwambia mwanasaikolojia wa gereza: “Hana nia ya kujiua.” Kauli hiyo inaibua maswali mengi leo. SEHEMU YA 4: Usiku wa Ajabu Kabla ya Kifo Agosti 9, 2019. Epstein aliachwa peke yake kinyume cha taratibu za gereza. Kamera mbili zilizokuwa zinaangalia selo yake hazikuwa zikifanya kazi. Walipaswa kumkagua kila baada ya dakika 30. Lakini walinzi hawakufanya hivyo. Baadaye iligundulika walikuwa wamelala. SEHEMU YA 5: Dakika Iliyotoweka Kulikuwa na pengo la dakika moja kwenye video. Baadaye iligundulika nakala kamili ya video iliharibiwa baada ya kesi kufungwa. Mashaka yalizidi. SEHEMU YA 6: Mwili Unapatikana Asubuhi ya Agosti 10 — Epstein alipatikana hana fahamu. Lakini: • Mwili ulikuwa baridi. • Selo ilionekana imevurugwa. • Ushahidi ulikuwa umehamishwa. Mpelelezi wa zamani alisema tukio lilionekana kama limepangwa. SEHEMU YA 7: Daktari Anayepingana na Ripoti Rasmi Mtaalamu wa uchunguzi wa maiti, Michael Baden, alisema majeraha ya shingo yalifanana zaidi na kunyongwa kwa nguvu kuliko kujiua. Hata kamba iliyopatikana haikuendana na majeraha hayo. SEHEMU YA 8: Kauli Rasmi vs Mashaka ya Umma Serikali ilihitimisha kuwa kifo kilikuwa kujiua. Lakini Mwanasheria Mkuu wa zamani alikiri kulikuwa na “makosa makubwa na uzembe wa ajabu.” Hadi leo, watu wengi wanaamini Epstein aliuawa. HITIMISHO Miaka imepita. Nyaraka mpya zinaendelea kutolewa. Maswali bado hayajajibiwa. Je, alikuwa mtu aliyekata tamaa? Au mtu aliyenyamazishwa kabla hajafichua siri kubwa? Ukweli kamili bado haujajulikana. Na kama kweli kifo cha Jeffrey Epstein kilipangwa... huenda waliohusika bado hawajawahi kuwajibishwa.

Share this post: