TheTanzaniaTime

Dkt. Mwigulu Afanya Ukaguzi wa Mradi wa Stendi Kuu ya Mabasi Arusha

2026-02-24 - 21:18

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba Februari 24, 2026 amekagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo Mikoani unaotekelezwa katika eneo la Bondeni City katika Halmashauri ya Jiji la Arusha. Mradi huo ambao utagharimu shilingi bilioni 14.3 una lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji na kupunguza msongamano katikati ya Jiji la Arusha. Mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika Mwezi Mei 2026 umefikia asilimia 49.

Share this post: