TheTanzaniaTime

CCM Yaipa Tano Serikali Ya Mapinduzi Zanzibar, Wananchi Wa Kikwajuni

2026-03-05 - 08:08

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na wakazi wa majumba ya Mjerumani Kikwajuni kwa kufikia maridhiano ambayo sasa yanatoa nafasi ya kuanza utekelezaji wa mradi ujenzi wa nyumba bora za kisasa ambazo zinatarajiwa kubadili mandhari ya Mji wa Unguja. Akizungumza na wanahabari waliofika ofisini kwake, leo 05 Machi 2026, CCM Kisiwandui kujua kinachoendelea kwenye mradi huo kutokana na kujitokeza sintofahamu baina ya baadhi ya wakazi na serikali, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema kufuatia maridhiano hayo mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani Milioni 45 sasa unaenda kutekelezwa. Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis Alisema tayari Tsh.Bilioni 1.8 zimelipwa kwa wananchi waliokuwa wakiishi katika nyumba zilizopo katika maghorofa hayo yaliyojengwa 1969 na nchi rafiki ya Ujerumani Mashariki ili wakatafute maeneo ya kupanga kwa muda wakati wa unatekelezwa wa mradi huo na watarudi kwenye nyumba hizo zikikamilika miaka miwili ijayo. Mwenezi Mbeto anabainisha kuwa wakazi wote wakiwemo waliokuwa wapangaji wa Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC), wamelipwa pesa za upangaji na wamepewa mikataba ya kurudi tena katika nyumba hizo zikikamilika. “Pale kuna nyumba 59 zinamilikiwa na wananchi kati ya 158 zilizopo na wote wamelipwa na wameanza kuondoka na hadi kufikia Jumapili huenda wote watakuwa wameondoka kupisha mradi na watarejea ukikamilika na utakuwa na nyumba 1095 bora za kisasa zenye miundombinu yote muhimu. Nyumba Zilizopo Katika Maghorofa Yaliyojengwa 1969 Na Nchi Rafiki Ya Ujerumani Mashariki Mwenezi Mbeto alibainisha kuwa kinachofanyika ndio maagizo ya CCM kwa serikali kuhusu wananchi wake hivyo chama kinawapongeza wananchi kwa kuelewa kusudio la kuletewa maendeleo na kuafikiana na SMZ chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Alisema licha ya chama kuagiza lakini pia kinasimamia kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa kulingana na makubaliano ya serikali na wananchi. Mwenezi huyo ambaye amewatoa hofu wakazi hao kwa kusema kuwa wote watarejeshwa kama mikataba waliyopewa inavyosema na kubainisha kuwa nyumba hizo ambazo zimeanza kubomolewa zinaenda pia kufungua utekelezaji wa miradi mingine ya makazi ya kimkakati katika miji yote ya Zanzibar ikiwemo Kilimani na Michenzani ambako majengo yake yamepitwa na wakati na ni chakavu.

Share this post: