TheTanzaniaTime

Burkina Faso Yashirikishwa Mbinu Bora za Utunzaji Mazingira na Ufugaji Migodi Tanzania

2026-02-17 - 08:19

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Ellen Maduhu, amekutana na Ujumbe kutoka Wizara ya Nishati, Madini, na Machimbo ya Burkina Faso uliofika Tanzania mnamo tarehe 8 Februari 2026 ili kujifunza kuhusu kufungwa kwa Migodi na Utunzaji Mazingira. Tangu Ujumbe huo uwasili hapa nchini, ujumbe huo umetembelea migodi kadhaa ikiwemo Mgodi wa Dhahabu wa Prime uliopo Nzega Mkoani Tabora ambao umefungwa tangu mwaka 2014, Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama ambao bado unaendelea na mchakato wa kufungwa, na Mgodi wa Dhahabu wa Geita. Zaidi ya hayo, walitembelea Wizara ya Madini na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), ambapo walijifunza kuhusu Sera na Miongozo ya Uchimbaji wa Madini, Kufugwa kwa Migodi, na Utunzwaji wa Mazingiraa. Aidha, ujumbe huo ulipata wasaa wa kutembelea kituo cha Afrika cha Madini na Jeolojia kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam na kuona shughuli zinazofanywa na Kituo hicho hapa nchini Ziara hiyo hapa nchini Tanzania inakamilika Februari, 16, 2026 ambapo wanatarajiwa kurejea nchini Burkina Faso tarehe 17 Februari, 2026.

Share this post: