TheTanzaniaTime

Brooklyn Beckham Aonesha Anasa Kupindukia, Divai ya Milioni 60 Yazua Gumzo!

2026-01-29 - 08:55

Brooklyn Beckham, ambaye ni mtoto wa kiume wa staa wa zamani wa mpira wa miguu, David Beckham, ameendelea kutikisa mitandao ya kijamii akiwa na mkewe, Nicola Peltz, kwa kuonesha maisha yao ya kifahari. Akiwa anakula bata, amechapisha picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa na mkewe wakifurahia chakula, huku pembeni kukiwa na chupa mbili za divai aina ya Château za mwaka 1831, ambazo zinaelezwa kuwa ni divai ghali zaidi duniani. Chupa moja inauzwa takribani pauni 17,000, sawa na shilingi milioni 60 za Kitanzania. Haya yanajiri wakati kukiwa na ripoti kwamba mkewe Nicola hupokea posho ya dola milioni 1 kila mwezi kutoka kwa baba yake, Nelson Peltz, ambaye ni bilionea mkubwa. Mtoto huyo wa Beckham, mwenye umri wa miaka 26 na anayejulikana kama influencer wa masuala ya upishi, aliibua vichwa vya habari hivi karibuni baada ya kuthibitisha hadharani kuwa mahusiano yake na wazazi wake, David na Victoria Beckham, yamevunjika. Taarifa hiyo ilitolewa kupitia tamko la kurasa sita lililosambazwa kwenye mitandao ya kijamii Jumatatu iliyopita, likieleza kwa kina mgogoro wa kifamilia uliotikisa familia hiyo maarufu duniani. Picha hizo zimechochea upya mjadala wa umma kuhusu maisha ya kifahari ya Brooklyn na Nicola, katika kipindi ambacho mvutano wa kifamilia pamoja na maswali kuhusu upendeleo, uhuru binafsi, na utajiri yanaendelea kuzunguka ndoa ya Beckham-Peltz

Share this post: