TheTanzaniaTime

BOT Yatangaza Nafasi za Kazi 83, Mwisho wa Kutuma Maombi Machi 24, 2026

2026-03-12 - 11:08

Serikali kupitia Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza nafasi 83 za ajira katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ikiwataka Watanzania wenye sifa kuomba nafasi hizo. NAFASI ZA KAZI BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) 10-03-2026 Baadhi ya Nafasi Zilizotangazwa Security Guard III – 13 Bank Officer III – 13 Accountant III – 8 IT Technician III – 6 Bank Examiner III – 6 Computer Analyst/Programmer III – 5 Internal Auditor (Systems Auditor) III – 4 Receptionist III – 4 Personal Secretary III – 3 Human Resource Officer III – 3 Legal Officer III – 2 Security Officer III – 2 Porter III – 2 Supplies/Procurement Officer III – 2 Kitchen Attendant III – 2 Mechanical Engineer III – 1 Electrical Engineer III – 1 Planning Officer III – 1 Financial Analyst III – 1 Electrical Technician III – 1 Electronics Technician III – 1 Business Analyst III – 1 Programmes Coordinator/Instructor III – 1 Masharti Muhimu ya Waombaji Mwombaji lazima awe raia wa Tanzania. Umri usizidi miaka 45 (isipokuwa kwa taasisi za kijeshi ambapo masharti ni tofauti). Waombaji waambatanishe vyeti muhimu kama: Cheti cha kuzaliwa Vyeti vya elimu na nakala za matokeo (transcripts) Vyeti vya taaluma au usajili wa kitaaluma (kama vinahitajika). Matokeo ya Form IV/VI slips hayakubaliki. Jinsi ya Kutuma Maombi Maombi yote yanapaswa kutumwa kupitia tovuti ya ajira ya serikali: http://portal.ajira.go.tz Mwombaji pia anatakiwa kuandika barua ya maombi kwa: Katibu Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma S.L.P 2320 Dodoma Mwisho wa Kutuma Maombi 24 Machi 2026 Ni waombaji watakaopitishwa kwenye mchujo pekee ndio watakaoitwa kwenye usaili.

Share this post: