TheTanzaniaTime

Benki ya Absa Tanzania Yadumisha Ushirikiano na Wateja Wake

2026-03-17 - 11:56

Benki ya Absa Tanzania imeendelea kuimarisha ushirikiano wake na wateja kwa kuandaa hafla ya futari iliyowakutanisha viongozi wa benki, viongozi wa dini, wafanyakazi pamoja na wateja, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, alisema benki hiyo inaendelea kuthamini uhusiano wake na wateja na wadau mbalimbali, huku akisisitiza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kukuza huduma bora za kifedha na maendeleo ya jamii. Miongoni mwa wageni waliohudhuria hafla hiyo ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omar, pamoja na viongozi wengine wa benki akiwemo Mdhibiti wa Masuala ya Fedha, Bw. Muhsin Kaye, na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere, pamoja na wafanyakazi na wateja wa benki hiyo. Hafla hiyo ya futari imeelezwa kuwa ni sehemu ya utamaduni wa Benki ya Absa Tanzania wa kuendelea kujenga ukaribu na wateja wake pamoja na kuimarisha mshikamano na jamii.

Share this post: