TheTanzaniaTime

Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar Pengo Afariki

2026-02-20 - 05:17

Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Cardinal Pengo, amefariki dunia jana Februari 19, 2026 majira ya saa 04:00 usiku akiwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam, kiongozi huyo wa kiroho ameitwa nyumbani kwa Baba wa Milele baada ya kuugua kwa muda mfupi, tukio lililoacha huzuni kubwa miongoni mwa waamini wa Kanisa Katoliki na Watanzania kwa jumla waliomfahamu kwa mchango wake mkubwa katika kulijenga Kanisa na taifa. Askofu Pengo atakumbukwa kwa hekima, unyenyekevu na juhudi zake katika kuimarisha mshikamano wa jamii pamoja na kusimamia maadili na amani nchini. Taarifa zaidi kuhusu ratiba ya mazishi zitatolewa mara baada ya maandalizi kukamilika. Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

Share this post: