Arsenal, Real Madrid na Paris Saint-Germain Watinga Robo Fainali UEFA
2026-03-18 - 05:53
Timu za Arsenal, Real Madrid na Paris Saint-Germain zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya UEFA Champions League baada ya kuonyesha ubora mkubwa katika michezo ya hatua ya 16 bora iliyopigwa usiku wa kuamkia leo. Katika dimba la Stamford Bridge, Paris Saint-Germain waliendeleza ubabe wao kwa kuichapa Chelsea mabao 3-0, na kufuzu kwa jumla ya mabao 8-2. Real Madrid waliendelea kuthibitisha ubora wao Ulaya baada ya kuifunga Manchester City mabao 2-1, na kufuzu kwa jumla ya mabao 5-1. Licha ya City kupata bao kupitia Erling Haaland, nyota wa Madrid Vinícius Júnior aliibuka shujaa kwa kufunga mabao mawili muhimu, likiwemo la ushindi dakika za mwisho. Kadi nyekundu ya Bernardo Silva iliathiri sana mipango ya Man City katika mchezo huo. Kwa upande mwingine, Arsenal waliendeleza kiwango chao bora baada ya kuifunga Bayer Leverkusen mabao 2-0, na kufuzu kwa jumla ya mabao 3-1. Ushindi huo unaweka matumaini makubwa kwa Arsenal ambao wanatafuta mafanikio makubwa barani Ulaya. FT: Chelsea 0-3 PSG (Agg. 2-8) 6′ Kvaratskhelia 14′ Barcola 62′ Mayulu FT: Man City 1-2 Real Madrid (Agg. 1-5) 21′ Silva 40′ Haaland 21′ Vinicius Junior 90+3′ Vinicius Junior FT: Arsenal 2-0 Bayer Leverkusen (Agg. 3-1) 36′ Eze 63′ Rice